Mfumo mpya unalenga kupambana na wafanyakazi bandia wanaopokea mishahara bila kufanya kazi
Maafisa wakuu nchini Kenya wamezindua mpango mpya wa
kuwasajili wafanyakazi wa serikali kwa njia ya kielektroniki, ili
kukabiliana na wafanyakazi ghushi wanaokula mishahara bila ya kufanya
kazi.
Serikali inasema kuwa maelfu ya wafanyakazi wa umma waliostaafu huendelea kupokea mishahara kwa njia ya udanganyifu.
Jambo hilo hugharimu serikali ya Kenya mamilioni ya dola kila mwezi kwa malipo yasiyostahili.
Taarifa ya serikali imesema kuwa wafanyakazi wa
umma wanahitajika kujisajili kielektroniki katika kipindi cha wiki mbili
zijazo, au hawatapokea misharaha yao.
Rais Uhuru Kenyatta aliahidi kupambana na rushwa katika sekta ya umma baada ya kuchukua usukani mwaka 2013.
Serikali ya kenya inaamini kuwa maelfu ya watu
hudai kulipwa mishahara kwa njia ya udanganyifu swala linaloigharimu
serikali takriban dola millioni 20 kwa mwaka.
katika visa vyengine wafanyikazi hupokea zaidi ya mshahara mmoja huku wafanyakazi waliokufa pia wakidaiwa kupokea mishahara.
Tatizo la wafanyikazi ghushi ni swala la kawaida katika mataifa mengi ya bara afrika.
Nigeria ilianzisha mfumo wa vitambulisho vya
kielektroniki wiki iliopita ili kukabiliana na swala hilo huku Ghana na
Senegal zikidaiwa kuanzisho mifumo kama hiyo
0 comments:
Post a Comment