Monday, September 22, 2014

Kesi ya mwimbaji wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha imepigwa kalenda kwa mara nyingine tena kwa sababu Hakimu anayeendesha kesi hiyo kupata shughuli nyingine nje ya ofisi.Mbasha alipanda kizimbani katika mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi yake hiyo ambapo mwendesha mashtaka Kiyoja Catherine aliahirisha kesi hiyo kutokana na Hakimu Williberforce Luwhego kupata dharura

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena 17 October mwaka huu ambapo Mahakama itaanza kusikiliza ushahidi ambapo upande wa mashtaka utakuwa na mashahidi wanne kwenye kesi hii inayomkabili mume wa Flora Mbasha anaekabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo ya ubakaji. SOMA ZAIDI>>

0 comments:

Post a Comment