Mechi za kutafuta tiketi za fainali za kombe la
mataifa ya Afrika mwakani huko Moroko ikiwa ni hatua ya makundi ambapo
Uganda imeutumia vema uwanja wa nyumbani wa Nelson Mandela kwa kuinyoa
Guinea mabao 2 kwa 0
Sudan ikicheza ugenini mjini Pwe Nwah imeambulia kipigo cha magoli mawili bila majibu kutoka kwa Jamhuri ya Kongo.
Bafana
Bafana ya Afrika kusini imebanwa nyumbani na mabingwa watetezi Nigeria
kwa kushindwa kufungana wakati Malawi imeinyuka Ethiopia 3-2 mjini
Blantyre.
Kwenye kundi C Angola wakashindwa kutamba nyumbani kwa
kichapo cha mabao matatu kwa 0 kutoka kwa Burkina Faso huku Lesotho
ikitoka sare ya bao moja moja na Gabon
Sierra Leone ikawahuzunisha
watu wake kwa kuiacha Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ichukue pointi
zote tatu kwa ushindi wa mabao 2 kwa 0, kama ilivyokuwa kwa Togo
iliyokubali kipigo cha mabao matatu kwa mawili kutoka kwa Ghana.
Mjini Praia…Cape Verde imeirarua Zambia 2 bila, Tunisia wakaitandika Misri 1 bila, nayo Msumbiji ikatoka sare ya 1- 1 na Niger
0 comments:
Post a Comment