Tuesday, September 9, 2014

Mtoto Happiness Kashinje (9) pichani kulia enzi za uhai wake.

MTOTO Happiness Kashinje (9) (pichani)aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Negezi mjini Shinyanga, ameokotwa akiwa amekufa baada ya kudaiwa kutekwa na watu wasiojulikana kabla ya kubakwa na kutobolewa macho.Tukio hilo lilijiri hivi karibuni Nhelegani, Kata ya Kizumbi kilometa chache kutoka nyumbani kwao.


Habari zilizofika Uwazi kuhusu mkasa huo zinasema, Happiness aliyekuwa akiishi na shangazi yake, alipotea Agosti 27, mwaka huu baada ya kuaga kuwa anakwenda saluni kupunguza nywele na hakurudi tena hadi  siku iliyofuata mwili wake ulipookotwa ukiwa umeanza kuharibika. 

0 comments:

Post a Comment