Rais Barack Obama wa Marekani ameidhinisha kupelekwa
vikosi vya wanajeshi wapatao 350 kwa lengo la kuwalinda wanadiplomasia
na wafanyakazi raia wa nchi hiyo waishio mji mkuu wa Iraq Baghdad.
Ikulu ya Marekani imesema wanajeshi hao
watakaopelekwa baadhi yao ni wale wanaojihusisha na diplomasia ya ulinzi
ya iraq ambao ni zaidi ya mia nane.
Hata hivyo Marekani inatarajia kuwatuma maofisa
waandamizi akiwemo John kerry katibu mkuu wa marekani na Chuck Hagel
katibu wa ulinzi ambao watakwenda mashariki ya kati katika harakati za
kuimarisha ushirikiano.
Hatua hiyo inafuatia vitendo vya mashambulizi na
mauaji yanayoendelea Iraq ikiwa ni matokeo ya utofauti kati ya Marekani
na makundi ya wapiganaji ambao wamekuwa wakiwalenga raia wa Marekani
waliopo nchini humo
0 comments:
Post a Comment