Wozniacki mefuzu kwa mara ya kwanza katika miaka mitatu iliyopita
Mcheza Tennis wa
Denmark,Caroline Wozniacki ameingia kwenye nusu fainali ya mashindano ya
tennis kwa kumshinda mchezaji bora wa 13 duniani Sara Errani wa Italia
kwa pointi, 6-0 6-1 .
Wozniacki, anayeorodheshwa wa kumi miongoni mwa
wachezaji bora zaidi duniani, alishinda mechi yake katika dakika 65 na
kujinyuakulia nafasi katika nusu fainali.
Bingwa huyo wa zamani wa dunia sasa
atacheza na Peng Shuai, wa China ambaye alifika nusu fainali yake ya
kwanza ya mashindano hayo kwa kumcharaza
Belinda Bencic wa Usiwizi kwa seti mbili za pointi 6-2 6-1.
Belinda Bencic wa Usiwizi kwa seti mbili za pointi 6-2 6-1.
Peng, mwenye umri wa miaka 28, alinukuliwa akisema amefurahi sana kwa kufika nusu fainali.
Katika mechi zengine za nusu fainali, ambazo
zitechezwa Jumatano, Serena Williams atamenyana na Flavia Pennetta huku
Victoria Azarenka akichuana na Ekaterina Makarova.
Wozniacki, ambaye ameingia katika nusu fainali
kwa mara ya kwanza katika miaka mitatu, alisema kuwa hii ni hatua kubwa
sana kwake.
"msimu huu umekuwa na misukosuko sana kwangu na kuweza kufika hapa najisikia vizuri sana
0 comments:
Post a Comment