Thursday, October 16, 2014

MCHUNGAJI anayejiita nabii na mtume, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) aliyetajwa kwa jina moja la Emmanuel amejikuta ndani ya majanga kufuatia madai mazito kwamba amemtorosha mke wa mtu ambaye ni mwimbaji wa Nyimbo za Injili Bongo anayekuja juu kwa kasi, Janet Mrema.
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Bongo anayekuja juu kwa kasi, Janet Mrema anayedaiwa kutoroshwa na mchungaji huyo. Kwa mujibu wa chanzo makini, mchungaji huyo alifika nyumbani kwa Jonas Mrema, mume wa Janet, maeneo ya Tegeta-Nyaishozi jijini Dar na kuishi kama mtumishi wa Mungu lakini polepole alianza mazoea tata na Janet. 

“Mume alianza kuhisi mabadiliko ya mkewe kwa mtumishi huyo, lakini nadhani aliona ni mawazo yake tu. Ndipo siku ya siku akashangaa mkewe na mchungaji huyo wameondoka nyumbani hapo. 
“Kwa sasa tangu tukio hilo litokee ni miezi kama mitatu. Mume alihangaika sana kumtafuta mkewe hadi jana (Jumatatu iliyopita) ndipo akampata wakiwa na mchungaji huyo kwenye nyumba moja ambako walikuwa wakiishi pamoja,” kilisema chanzo chetu.SOMA ZAIDI HAPA>>>

0 comments:

Post a Comment