"Kumetokea
ajali mbaya mida hii maeneo ya Jeti Lumo mwisho wa lami ambapo gari
kubwa la mizigo limeangua daladala iliyokuwa kituoni.
Ajali hiyo
imetokea wakati gari hilo semi-trailer ikikata kona pale mwisho wa lami
ambapo kontena lilianguka na kutua juu ya bodi ya daladala.
Mtoa
taarifa wangu amesema hali ni mbaya na bado hajajua idadi ya vifo na
majeruhi ujumla.Pia gari imepondeka sana jambo ambalo linaashiria hatari
zaidi.
Kuna gari la kunyanyua
makontena limeshafika pale lakini limeshindwa kutoa msaada wa uhakika
kutokana na kuzidiwa uzito na kontena ambapo likijaribu kunyanyua
kontena ushuka chini na kuzidi kuongeza maafa."
More updates to come...
0 comments:
Post a Comment