Re: Boss wa Home Shopping Centre 'apewa shavu' na Tanzania huko China
Extraterrestrial:
Umefanya vizuri kutoa ufafanuzi ulioutoa. Umejaribu kutoa ufafanuzi kwa hoja tofauti na wale tu wanaoona kuwa wanaohoji uteuzi huu wana chuki na dini fulani. Kwao wao haijalishi hata kama aliyeteuliwa ni jambazi, alimuradi tu awe ni muumini wa dini wanayoiamini. Lakini ufafanuzi wako haujakamilika.
1. Weka ushahidi hapa kuthibitisha utaratibu na sifa za mtu anayeweza kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa "Honorary Consular". Kututaka tu-Google ni kututania kwa kuwa kuna uchafu mwingi kwenye mtandao.
2. Hoja: Huyu kijana hana sifa za kuiwakilisha nchi hii kwenye jambo lolote lile kwa kuwa anatiliwa shaka sana na jamii. Mienendo yake,jamaa zake, na washirika wake serikalini (ikiwa ni pamoja na Serikali ya Uchina? Maana hufanikishi jambo China bila mlungula.)ni ya kutia shaka. Thibitisha kuwa kijana huyu ana sifa za kuteuliwa kuwa "Honorary Consular". Kusema tu ni mfanyabiashara haitoshi maana wafanyabiashara wapo wengi. Thibitisha kuwa kijana aliyeteuliwa "anaelewa vizuri foreign policy" za Uchina. Pia naomba kujua anashughulika na biashara gani haswa? Mapato ya kampuni yake kwa mwaka ni kiasi gani? Je, ni Mtanzania na analipa kodi Tanzania? Rekodi yake katika hilo ikoje? Au kwa kuwa Serikali haimlipi mshahara (kwa maana nyingine anajitolea?) hatuna haki ya kuhoji? Je, unaamini kuwa huyu kijana anajitolea and he is not getting anything in return other than "privileges and immunities"?
3. Kazi ya "Honorary Consular" ni nini? "Mara nyingi hawalipwi mshahara". Je, huyu atalipwa mshahara?
4. Fafanua ni jinsi gani kijana huyu atafanya "nchi na wananchi kunufaika"? Je, kama Mhe. Rais asingemteua kijana huyu kuwa "Honorary Consular", "nchi na wananchi" wangepata hasara gani?
5. Ukweli kwamba "Honorary Consular" anaripoti kwa balozi si sababu ya kuwafanya watu waache "kulalama" . Kama kuna walakini kwenye jambo lolote, ni vizuri watu wakahoji. Hii tabia ya kutaka watu kukaa kimya tu bila kuhoji masuala mbalimbali ni ya kiimla na inapaswa kukemewa kwa nguvu zote. Demokrasia na ustawi wa jamii huchangiwa na watu kuuliza maswali. Hukuwashirikisha wakati wa kuteua, hivyo wana haki ya kuhoji. Kwa nini unadharau watu kwa kuuliza maswali yanayohusu mienendo ya viongozi wao? Au ndio mmeshajimilikisha hii nchi?
6. Je, kijana anayeonekana kwenye picha na mabastola ndiye huyu ameteuliwa kuwa "Honorary Consular"?
7. Ni "privileges and immunities" gani nchi hutoa pindi "Honorary Consular" anapokuwa si raia wa nchi anayoiwakilisha?
8. "Honorary Consular" hahitaji vetting. Hii ina maana anayeteua anaweza kuteua hata Sicilian Don au jambazi lolote lile kuwa "Honorary Consular"?
With The permanent secretary in the ministry of foreign affairs and international cooperation Mr. John Haule
Msiniulize vetting ya yeye kupewa Ubalozi huko Guangzhou China ilifanya lini, na nani na criteria zipi alizokuwa nazo huyu mwarabu wa Yemen mpaka kupewa Ubalozi.
1. Huyu jamaa hakufayiwa vetting yoyote ile whatso ever na usalama wa Taifa kabla hajapewa hiyo nafasi.
2. Familia yake na biashara zao zimekuwa kwenye kashfa nzito nzito za kwa ukwepaji kodi
3. Salaah hana elimu wala qualification yoyote ile ambayo ingemfaya apewe nafasi hiyo. As a matter of fact how can you give a diplomatic post kwa mtu ambaye kaishia standard 6?
4. Kwa sababu za kiusalama aka national security hafai kupewa hiyo nafasi.
5. Kwa sababu za national interest hafai kupewa hiyo nafasi
6. Foreign wapo watu wengi sana ambao wana qualify kupewa hizo nafasi na washapitia hiyo vetting na due dilligence
7. Salaah na familia yake hawana intergrity -both professionally and personally kuwa ma diplomats wa tanzania kokote kule duniani
Kuna vijana wengi wa Kitanzania ambao wamesoma,wazalendo na washafanyiwa vetting na usalama na wapo Foreign hawapewi
Sasa cha kujiuliza hibi serikali ya nchi hii ina maana gani kusomesha watu wake na kisha kuwaweka benchi pale foreign halafu wanaenda kumteua huyu mshihiri wa Yemen ambaye hakusoma kuwa balozi wetu huko china?
Mbaya zaidi utashangaa jinsi mawaziri na viongozi wa juu wa serikali wanavyo mnyenyekea wakati kuna vijana wa Kitanzania ambao wasomi wanaendelea kusota pale wizarani na nafasi hizi hawapewi.
From the left side Commissioner of Immigration Hon. Ambokile, SALAAH in the middle and Inspector General of Police Mr. Mangu
with his friend Samuel Sitta on Emirates First Class
Tuesday, October 28, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment