Watu sita wakiwamo wahudumu watatu wa afya wa hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, wamewekwa chini ya uangalizi maalum baada ya kumhudumia mgonjwa aliyefariki akiwa na dalili za ugonjwa wa ebola.Mtu aliyefariki alitajwa kuwa ni Salome Richard (17), anayetoka katika kijiji cha Kahunda wilayani Sengerema.Akithibitisha kuwapo kwa hali hiyo Mganga Mfawidhi wa
Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema, Dk. Mary Jose, alisema mgonjwa huyo alifikishwa katika hospitali hiyo na ndugu zake watatu akiwa na homa kali huku akitokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili wake.Alisema vipimo vya mgonjwa huyo vimepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
“Tulimpokea juzi saa 7 mchana kutoka katika kijiji cha Kahunda wilayani hapa akiwa na homa kali akitokwa damu mwilini, lakini kwa tahadhari tulimweka wodi maalum peke yake akipatiwa matibabu na ilipotimu saa 8 usiku alifariki dunia,” alisema
Alisema kutokana na tahadhari ya ugonjwa huo, watumishi watatu wa idara ya afya na ndugu watatu wa marehemu huyo, wamezuiliwa kwa kuwekwa katika uangalizi maalum hadi matokeo ya vipimo vilivyochukuliwa vitakaporejeshwa toka Muhimbili.SOMA ZAIDI>>>

0 comments:
Post a Comment