
MMH! Majanga! Mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Juliet Gaison Komba (37), mkazi wa Mbagala Kuu, Temeke, Dar hivi karibuni amekutwa na mauti akiwa Gesti ya Kigoma, Mbagala Charambe, Dar.
Waombolezaji wakilia kwa unchungu kanisani.Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, mwanamke huyo ambaye mumewe ni kigogo mwenye cheo cha mkurugenzi wa kampuni moja ya usafirishaji jijini Dar, alikutwa na mauti baada ya kuingia kwenye gesti hiyo na mwanaume mmoja aliyedaiwa kuwa ni hawara yake licha ya kuwa na mume.
Mmoja wa wahudumu wa gesti hiyo, Nickson John alisema siku ya tukio, mwanamke huyo na jamaa yake aliyevaa kofia maarufu kwa jina la kapelo, walifika kwenye gesti hiyo saa saba mchana.
Alisema: “Waliulizia chumba chao cha siku zote maana walikuwa wakifika kila wakati, nikawaambia kiko wazi.
0 comments:
Post a Comment