Tuesday, October 21, 2014

HALI bado tete! Polisi wa Kituo cha Magomeni jijini Dar, wamemkamata baba mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Omar baada ya kupokea kipigo ‘hevi’ kutoka kwa raia wenye hasira kali akihusishwa na utekaji wa denti wa Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere iliyopo maeneo hayo.
Denti wa Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere, Magomeni (mwenye sare za shule) aliyenusurika kutekwa na njemba inayotambuliwa kwa jina moja la Omar.
Tukio hilo lililokusanya kadamnasi lilijiri wikiendi iliyopita, Magomeni-Kagera, Dar wakati mwanafunzi huyo akitokea shuleni.Kwa mujibu wa mashuhuda, denti huyo alipofika eneo hilo, baba huyo alimsalimia na baada ya kujibiwa salamu yake alianza kumchombeza kwa maneno matamu-tamu.PICHA ZAIDI>>>>

0 comments:

Post a Comment