Mmoja wa mapacha wa kundi
la P-Square, Peter Okoye amechaguliwa kuwa balozi wa Olympic Milk.Dili
hilo linadaiwa kuwa la mamilioni ya naira. Hii ni mara ya kwanza kwa
mmoja wa ndugu hao kusaini mkataba wake mwenyewe kwakuwa mikataba mingi
husaini pamoja.
Wafuatiliaji wa burudani nchini Nigeria wanahisi hiyo inaweza kuwa ni dalili ya kutokuwepo maelewano mazuri kati yao. Kwenye tangazo la maziwa hayo, anaonekana Peter peke yake.
0 comments:
Post a Comment