.jpg)
Ifuatayo
ni update ya msiba wa mdogo wake Mwenyekiti wa African Stars
Entertainment (ASET) Baraka Msiilwa, Marehemu Furaha Ramadhani Baraka,
kilichotokea wikiendi iliyopita huko Ubelgiji.
Taarifa
ni kwamba mwili wa Marehemu mdogo wetu Furaha unaondoka Brussels kesho
usiku kwenda Zurich. Utalala Zuruch na kusafirishwa Jumatano Asubuhi
kwa ndege ya shirika la Swiss Air, na unatarajiwa kuwasili Dar es salaam
siku hiyo hiyo ya Jumatano mnamo saa mbili usiku
Mazishi
yamepangwa kufanyika siku ya Alhamisi milango ya Alasir katika
Makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam baada ya kuuswaliwa katika
Mskiti wa Maamur Upanga. Msiba upo nyumbani kwa marehemu mama yetu
Kinondoni Hananasif/ Mkwajuni hapa Dar es salaam.
Habari
hizi ziwafikie ndugu, jamaa, jirani na marafiki popote pale walipo.
Tuzidi kumuomba Mola aiweke roho ya mareheme mahala pema peponi
0 comments:
Post a Comment