MACHO YAELEKEA KWENYE UZINDUZI NCHINI TANZANIA!
Dar es Salaam, 28 October- Kampuni ya Samsung imezindua toleo jipya la simu zake za Galaxy Note 4 Jijini Berlin Nchini Ujerumani Septemba 2014. Toleo hilo la teknolojia ya kisasa katika orodha za simu aina ya Note inazidi kuimarisha kampuni ya Samsung na kuzidi kufanya vizuri katika soko la simu duniani. Siku ya tarehe 17 Octoba, 2014 Kampuni ya Samsung ilifanya uzinduzi Mjini wa Cape Town- Afrika Kusini katika ziara ya Galaxy Note 4 Barani Africa.
Watanzania wanatarajiwa kupanga mistari katika maduka ya Samsung kushudia toleo jipya la simu katika familia ya Galaxy Note. Hii inatokana na uzinduzi mkubwa uliyofanyika Cape Town-Afrika Kusini ambayo ilikua ni ishara ya upatikanaji wa simu hizi za kisasa katika soko la Bara la Afrika na Tanzania ikiwemo.
Kutokana na Uzinduzi mkubwa uliofanyika Berlin, simu hii imepata umaarufu mkubwa na kujulikana kama ‘‘muongozi wa mabadiliko katika ulimwengu wa simu (smartphones) za mkononi’’. Galaxy Note 4 mpya ina kioo kikubwa chenye ubora zaidi wa kuonyesha matukio, na kalamu (S Pen) ya kipekee inayompa mtumiaji uhuru na uwezo mkubwa wa kutumia simu hiyo.
Uzinduzi Barani Afrika Ulihusisha viongozi mbalimbali wa kampuni ya Samsung duniani akiwemo Mh. Mike Seo Mkurugenzi Mtendaji wa Samsung Electronics Tanzania, pamoja na mawakala wa Samsung, waandishi wa Habari na washiriki wengine. Continue reading →
0 comments:
Post a Comment