Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Mwanadamu ameumbwa na kuzaliwa akiwa na asili ya kuwa na uwezo na upeo unaomuwezesha kuwasiliana baina ya mtu na mtu kunzia ngazi ya familia, jamii inayomzunguka, taifa na hatimaye ulimwengu mzima.
Akiwa na mamlaka ya kutumia mawasiliano katika maisha yake ya kila siku, mwanadamu anayatumia mawasiliano hayo kama mchakato wa kuhamisha na kupashana taarifa ama habari kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa nyakati tofauti tofauti.
Mchakato huo wa mawasiliano unaweza kuwa ni mwingiliano unaohusisha ishara kati ya angalau wakala wawili walio na mkusanyiko wa ishara na sheria za elimu ishara.
Kwa mantiki hiyo, mwanadamu anatumia mawasiliano kwa kupasha au kubadilishana mawazo, maoni, au habari kwa kunena, maandishi, au ishara.
Historia inasema, mawasiliano yamekuwepo tangu kuwepo mwanadamu hatua inayoleta mantiki kuwa mawasiliano yamekuwa kongwe kama jamii ilivyo kwani yamekuwepo tokea enzi za mababu.
Mwanadamu anatumia mawasiliano katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku kulingana na wakati husika.
Ndani ya mchakato wa kuhabarisha, habari husika hupakiwa, kutumwa na kupashwa na anayetuma kwa anayepokea kupitia kwa njia maalum kulingana na mahali na wakati husika.
Mawasiliano yakishatumwa, anayepokea hupakua ujumbe ule na kumpatia aliyetuma jibu ama majibu ya alichotaka kujulishwa ambapo mawasiliano yanahitaji anyetuma ujumbe na anayepokea wapate mrejesho unaoonesha kumekuwa na mawasiliano sahihi kulingana na mtoa ujumbe.
0 comments:
Post a Comment