Monday, October 13, 2014

MBUNGE wa Jimbo la Urambo Mashariki Samwel Sitta, amepokelewa kwa kishindo Jimboni kwake Urambo na kuhutubia katika Viwanja vya Mwananchi Square.
Sitta akihutubia wapigakura wake alielezea jinsi mchakato wa Bunge Maalum la Katiba ulivyokwenda hadi alipokabidhi Katiba inayopendekezwa kwa Rais Dkt.Jakaya Kikwete.
Katika hotuba yake hiyo, Sitta ambaye alikuwa Mwenyekiti wa bunge hilo, alielezea jinsi katiba ilivyotoa haki za wakulima, wafugaji, haki za watoto, baraza la vijana la Taifa, hamsini kwa hamsini kwa wanawake katika nafasi za uongozi na mengineyo.

Aidha, amewataka wana Urambo na watanzania kuipitia Katiba inayopendekezwa kwa kina na ufasaha kwani imekidhi vigezo na matakwa ya wananchi yenye maslahi mapana ya vizazi kwa vizazi.

0 comments:

Post a Comment