Posted by Williammalecela.com on Thursday, December 11, 2014
Aliyekuwa Miss Tanzania (2006), Mwigizaji na mkurugenzi wa kampuni ya Endless Fame, inayojishughulisha na mambo ya filamu hapa nchini, Wema Sepetu aka Madame hivi sasa yupo nchini Ghana kwa ajili ya kufanya kazi na msanii maarufu nchini humo na Afrika kwa ujumla aitwaye Van Vicker.
Leo hii kwenye mtandao wa kijamii Wema aliweka picha hiyo akiwa na msanii huyo na kuandika “In the Making” na kumtag Van.
Jina la project (MOVIE) hiyo mpya hadi sasa bado halijajulikana. Endelea kutufuatilia hapa tutakujuza.
0 comments:
Post a Comment