Posted by Williammalecela.com on Friday, December 12, 2014
JAMBO
limezua jambo! Mapigano ya wakulima na wafugaji wa jamii ya kimasai
yaliyotokea hivi karibuni katika Kitongoji cha Dumila, Wilaya ya Kilosa
mkoani hapa yamewakurupua wazinzi waliokuwa wakifanya uchafu wao katika
nyumba ya kulala wageni.
Binti
akiwa ndani ya chumba cha gesti. Mwanahabari wetu aliyenasa tukio hilo
lililotokea Desemba 9, mwaka huu, alimshuhudia dereva wa lori ambaye
jina lake halikuweza kupatikana mara moja, akitoka katika gesti maarufu
eneo la Dumila akiwa na nguo ya ndani huku binti aliyekuwa akibanjuka
naye akikurupuka na taulo ambapo nguo zake za ndani na mazagazaga yake
alicha chumbani.
Gesti
iliyovunjwa vioo. Kwa mujibu wa chanzo chetu, mapigano hayo yaliyodumu
kuanzia saa 4 asubuhi hadi 10 jioni, yaliibuka baada ya mmasai huyo
kumkata mkono mkulima katika mashamba ya Kijiji cha Mteteni alipokuwa
akimzuia kukata majani shambani kwake.
Chanzo hicho kilizidi kudai kuwa, baada ya wakulima kuona mwenzao
amekatwa mkono, walijikusanya na kuwavamia wafugaji hao ili kulipa
kisasi.
Nguo
za ndani zilizoachwa. “Wamasai baada ya kuzidiwa nguvu na kundi hilo la
wakulima, waliamua kukimbilia msituni ambapo baada ya kuwakosa,
wakulima hao waliamua kufunga barabara kuu ya Morogoro-Dodoma
inayokatiza kwenye Kitongoji cha Dumila kushinikiza serikali ya wilaya,
mkoa na taifa kuwaondoa wamasai kwenye wilaya yao,” kilieleza chanzo
hicho.
Polisi
wakiwa eneo la tukio. Wakati hayo yakiendelea ndipo vijana wanaodhaniwa
kuwa ni wa kutoka katika jamii ya wakulima walipoamua kuvamia gesti na
nyumba za wamasai kisha kuvunja vioo vya madirisha na baadaye kuvunja
mlango.
Vijana
waliokamatwa na polisi. Mbali na dereva wa lori na kiburudisho chake
ambacho pia hakikujulikana jina lake kukurupuka katika gesti hiyo,
mwandishi wetu alishuhudia wateja wengine wakitimka wakiwa watupu huku
wengine wakiwa wameshikilia nguo za ndani mkononi.
0 comments:
Post a Comment