Tuesday, January 20, 2015


Msanii ambaye pia ni msambazaji wa kazi za wasanii, William Mtitu.UPEPO ulichafuka! Katika hali ya taharuki, msanii ambaye pia ni msambazaji wa kazi za wasanii, William Mtitu amenusurika kipigo wakati wa kikao cha wasambazaji kujadili bei ya CD za kazi za wasanii. Kikao hicho kilifanyika wiki iliyopita katika Ukumbi wa Habari Maelezo, Posta jijini Dar kufuatia kampuni ya usambazaji ya Steps Entertainment kutangaza kuuza CD kwa shilingi 1,000 badala ya 3,500 ya awali kwa kigezo cha kukwepa maharamia.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Mtitu alinusurika kupokea kichapo hicho mara baada ya kuhoji uhalali wa waongozaji wanaodaiwa kuwa wanafanya kazi na Kampuni ya Steps kuvamia kikao hicho.
Chanzo hicho kiliendelea kueleza kwamba kabla ya kikao hicho kilichokuwa na lengo la kupinga bei ya Steps hakijaanza, Mtitu alisimama na kuhoji kwa nini waongozaji wa Steps wahudhurie badala ya wasambazaji husika?
Baada ya Mtitu kuhoji suala hilo, waongozaji hao ambao majina yao hayakupatikana mara moja, walimjia juu huku wakitaka kumpiga jambo ambalo lilizua zogo na kusababisha kikao hicho kusambaratika.“Mtitu anatetea sana haki za wasanii hivyo alipoona waongozaji wa filamu wa Steps na baadhi ya wasanii kama Niva wamevamia kikao hicho akahoji kwani waliambiwa kwenye kikao hicho wanaotakiwa kuwepo ni wasambazaji pekee, hapo ndipo timbwili likaanza,” kilisema chanzo hicho.

William Mtitu akipozi. Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Mtitu ili kujua ukweli ambapo alisema:
“Kweli tulikuwa na kikao cha wasambazaji lakini kilivurugika, kuhusu kunusurika kupigwa, wasingeniweza.”

Jitihada za kuupata uongozi wa Steps kuzungumzia tukio hilo hazikuzaa matunda kwani hawakupatikana hewani. Jitihada zinaendelea.

Vurugu hizo zilizovunja kikao hicho zilishuhudiwa pia na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Siamon Mwakifwamba ambaye alihudhuria kikao hicho.

0 comments:

Post a Comment