| COUTINHO AKISHANGILIA BAADA YA KUFUNGA BAO KWENYE UWANJA WA AMAAN, ZANZIBAR, LEO. |
Yanga sasa haikamatiki kwani ukiwasogelea, unakula zako nne.
Baada ya kuitwanga Taifa ya Jang'ombe kwa mabao 4-0 katika mechi ya
Kombe la Mapinduzi, wamefanya hivyo tena kwa Polisi Zanzibar.
Katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, Yanga ilipata
mabao yake kupitia Andrey Coutinho aliyefunga mawili, Kpah Sherman na
Simon Msuva.
Yanga ingeweza kufunga mabao mengi zaidi kutokana na kuutawala mchezo,
lakini mara kadhaa wachezaji wake hawakutulia kwenye umaliziaji.
Wakati mwingine Polisi Zanzibar walilazimika kucheza kibabe ili
kuwapunguza kasi wachezaji wa Yanga ambao walifunga mabao mawili kwa
kila kipindi.

0 comments:
Post a Comment