Mwaka huu wa 2015, ni mwaka wa uchaguzi mkuu, ni mwaka ambao kama taifa tunatagemea kupata amir jeshi mkuu mpya na rais wa awamu ya tano wa jamhuri yetu. Vyama mbalimbali vya siasa vinapambana na kujiandaa kuhakikisha kuwa amir jeshi huyo anatokana na wao. CCM kama chama tawala kinajiandaa kwa hili na upo mnyukano mkubwa ndani ya chama wa kuhakikisha kuwa anapatikana Rais Bora na Mwenyekiti muadilifu wa Chama hicho.


Vijana katika sehemu zote, katika taasisi hizi za kisiasa wamekuwa ndio wachakalikaji wakubwa, ndio wapiga debe wa wagombea mbalimbali ambao wamekwishatangaza nia na wale ambao bado nia yao haijawekwa wazi. Kwenye Mitandao ya kijamii, katika magazeti, wordpress na kwingineko vijana wanachuana kuwapamba wagombea wao.


Vijana ndani ya Chama cha mapinduzi wamekuwa katika vita baina yao inayotokana na makambi yao ya wagombea urais.,vita hii inatokana na imani kubwa waliyonayo kuwa ukifanikiwa kusimama ndani ya CCM kama mgombea basi bila kipingamizi chochote huyo ndie anayekuja kuwa Rais wa Jamhuri kwa awamu ya tano.


Hali ni tofauti kabisa kwa upande wa Upinzani, kwani kwao hakuna vuguvugu za wagombea Urais na wote wamejielekeza kwenye majimbo kutokana na ukweli kuwa hakuna tumaini la kushika dola kwa upinzani. Na hivyo basi vijana wa Chadema, Cuf na NCCR wamejikita katika kupigania na kuwapambanua wagombea watokanao na CCM..kwenye bunge la jamhuri wapinzani wanapigana vita ya wagombea wa CCM, tumbili na wenzake wamejipambanua wazi kuwa wao ni wa kundi moja wapo la urais ambalo mgombea wake ni wa CCM.,kwenye mitandao ya kijamii akina Yericko Nyerere hawaandiki tena kuhusu ziara za Babu na mkewe, wala hawaandiki kuhusu mnyika na porojo zake, hawaandiki chochote zaidi ya wasifu wa wagombea Urais ndani ya CCM, Kitila Mkumbo na wenzie katika waandishi waliokuwa wakiibeza CCM kila kukicha wamejikita katika kuandika Ubora wa wagombea wa CCM, ni ajabu lakini ni kweli kuwa wasomi hawa ambao wanaona CCM imepoteza dira lakini wanaona katika CCM wamejaa wenye uelekeo.,ni ajabu.


TanzaniaDaima kama chombo kikuu cha Chama katika kuripoti taarifa zake, kwa mfululizo tangu mwaka umeanza front page zake zimejaa wagombea wa CCM na sarakasi zao, Mbowe, Slaa na Wengineo sio tena ajenda ya wahariri katika chombo hicho. Inafurahisha, Mbowe amefanya tukio la kuandaa vijana 4000 wa red brigades na Tanzania Daima imekuja na front page news “HUKU LOWASA, KULE MWIGULU” Ikasema >wabunge 150 CCMwampigia debe lowasa, yeye amwachia Mungu., >utafiti wamuibua Mwigulu kuwa Kinara wagombea Vijana. Hii ni raha ya roho.


Hali hiyo ni kielelezo cha ukweli kuwa Vijana ndani ya Chadema na Ukawa kwa ujumla wamepoteza matumaini na vyama vyao na viongozi ndani ya vyama vyao, hawawaongelei tena wala hawawafikirii kuwa wanaweza kuwa ni Viongozi wa Jamhuri yetu ya Tanzania. Zamani kidogo matumaini yalikuwepo tena makubwa, tuliamini kuwa Slaa anaweza kuchukua nchi,tuliamini CCM wameshinda kwa kuiba kura na kupitisha makontena ya karatasi za kura. Vijana tuliimba wimbo wa matumaini mapya, hata mimba ya mke wa Slaa kwetu ilikuwa ni ajenda, kuwa Babu ni Kidume haswaa. Leo hali ni tofauti, Tafiti hazitaji tena kuwa wapo wapinzani wenye nguvu, Tafiti zinasema CCM maarufu, zinataja orodha ya wanaCCM tu katika wanaodhaniwa kumrithi JAKAYA, hawatajwi wapinzani.


Hii ni HALI HALISI.,na hizi ndizo salamu zangu kwenu kwa mwaka 2015..JIPANGENI.