KIMENUKA! Beautiful
Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’ amemporomoshea matusi mazito shemeji wa
Zarina Hassan ‘Zari’, King Lauwrance akidai amemuudhi sana kwa kitendo
cha kuvujisha picha inayomuonesha akiponda raha nchini Afrika Kusini
‘Sauz’ na mume wa Zari, Ivan Semwanga, Risasi Mchanganyiko linakupa
mchapo kamili.
Mwishoni mwa
wiki iliyopita, Wema na staa wa Bongo Fleva, Omari Nyembo ‘Ommy Dimpoz’
walikwenda Sauz kurekodi video ya wimbo wa msanii huyo ambao jina lake
bado halijafahamika mara moja ndipo baadae picha ya Ivan, Wema na King
Lawrence ilipovuja na kuzua gumzo.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichokuwa Sauz, baada ya Wema na Ommy kutua nchini humo na ‘project’ hiyo ya video, King Lawrance alidaiwa kuandaa mpango kabambe wa kuhakikisha kwa namna yoyote wanaonana na Wema kisha kupiga naye picha ambayo akiivujisha mtandaoni kila mtu ataamini wamefanya malipizi kwa zilipendwa wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye amemnyakua Zari, mke wa Ivan.

“Ilikuwa ni
mpango wa malipizi, King na Ivan walikuwa wanaumia moyoni kumuona
Diamond anatoka na Zari wakati wao wana fedha kuliko Diamond hivyo
waliposikia mtoto wa kike (Wema) yupo Sauz wakasema watadili naye hadi
kieleweke, iwe ni kwa kufanikisha zoezi la kutoka naye kimapenzi au hata
kupiga picha ambazo zikisambaa mitandaoni, watu watajua kwamba
wamefanya malipizi,” kilisema chanzo chetu.
KING AFANIKIWA KUIVUJISHA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, baada ya kufanya project, Ommy na Wema usiku walikwenda katika moja ya klabu kula bata ndipo King na Ivan walipozama na kufanikiwa kupata picha na Wema wakiwa katika kochi moja kisha akaitupia katika mtandao wa Istagram.

WEMA ACHARUKA
Baada ya picha za Wema na Ivan kusambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, mwandishi wetu alimtafuta Wema kwa njia ya simu ambapo alimcharukia King kwa matusi mazito ambayo kimaadili hayandikiki gazetini hata mtandaoni.

“Yule
ni...(tusi) ameniboa kweli...(tusi) unajua vitu vingine vya kipuuzi
kabisa, wanatafuta kiki zisizokuwa za msingi wa...(tusi)” alisema
Wema.Wema alisisitiza kuwa hataki kumzungumzia sana King kwani anaamini
akifanya hivyo atamuongezea umaarufu ambao amekuwa akiutafuta muda
mrefu.
King Lawrence
amekuwa akimtusi Diamond mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii huku
akionesha jeuri ya fedha kwa kile kinachoonekana kuumia kwake roho kwa
kijana wa Tandale kumchukua shemeji yake Zari, aliyezaa na Ivan watoto
watatu.

0 comments:
Post a Comment