Saturday, February 28, 2015

DSC_01311-1024x681 (1)
Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mh. Alexandre Lévêque akimkabidhi tuzo ya kwanza Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania-TAMWA,Bi. Valerie Msoka kwa kufanikisha kampeni dhidi ya ndoa za utotoni.
Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (TAMWA) Valerie Msoka, amekuwa mtu wa kwanza kutunukiwa tuzo ya CEFM Champion, na Ubalozi wa Canada nchini.
Katika sherehe fupi iliyofanyika Serena Hotel 24 Februari 2015, Balozi wa Canada nchini Bwana Alexandre Leveque alisema kuwa Valerie Msoka amekuwa mwanaharakati wa kwanza kutunikiwa tuzo hiyo na ubalozi wake kama ishara ya kukubali mchango wake kupiga vita ndoa za utotoni, za kulazimishwa na ukeketaji kwa watoto wa kike nchini.

“Watoto wa kike na wanawake wamevumilia machungu ya ndoa za utotoni na za kulazimishwa hivyo wanahitaji mtu wa kuwasemea: mtu ambae ataelezea taarifa zao zinakazosaidia kuwaweka watu pamoja na kuleta mabadiliko yenye tija,”amesema Balozi Lévêque. Valerie Msoka atakuwa mtetezi. Ninafuraha kumtangaza kuwa Mtetezi wa CEFM wa Ubalozi wa Canada nchini Tanzania.”
Valerie ametumia ujuzi wake kama mwanahabari aliyebobea, mwanaharakati na mpenda maendeleo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali bila kujali litakalomtokea au kueleweka vibaya na jamii.
Ameandika taarifa zenye kuvuta hisia, huruma na kuhamasisha kasi ya mabadiliko Katika jamii na watunga sera,” alisema Balozi Leveque.

0 comments:

Post a Comment