Friday, March 20, 2015



MAKINDA AIONEA HURUMA CHADEMA.

By Ole Mushi.


Kama mlivyosikia Jana kuwa Zitto kabwe angelihutubia bunge na kuwaaga wabunge wenzake baada ya miaka kumi ya Utumishi na uzalendo uliotikuka kwa watanzania.

Kama ilivyokawaida ili upewe fursa ya kufanya hivyo ni lazma uwasilishe hotuba yako kwa uongozi Wa bunge waipitie halafu upewe fursa ya kufanya hivyo. Hata hivyo Zitto alizuiwa kufanya hivyo baada ya mama makinda kuisoma hatuba ile na kwa kushauriana na uongozi Wa bunge kwa pamoja walimtaka Zitto kwenda kuirekebisha kwa ustawi Wa demokrasia nchini.

Katibu mmoja Wa bunge alidokeza kama hotuba ile ingesomwa pale bungeni na wanachi wakaisikia Leo chadema ingekuwa imebaki na viongozi wake tu huku wanachama wote wakiwa wamerudisha kadi zao.

Ndani ya hotuba hiyo ambayo ameiandaa Zitto akishirikiana na swahiba wake prof kitila pamoja na wanazuoni wengine ambao nimewaihifadhi majina yao kwa sababu maalaumu wameichambua na kukivua chama nguo katika kipengele walichokiita CHADEMA WASIOIJUA WATANZANIA.

Katika kipengele hicho kumeanikwa maovu ya Yale wafuasi Wa chadema wasichokijua kuhusu chama chao. Aidha katika kipengele hicho kimeanza kwa kunukuu waraka ule waliouandika kina mwigamba. Spika amemtaka Zitto kurekebisha kipengele hicho.

Hata hivyo hatuba hiyo imeanza kusambaa kwa wabunge bila marekebisho yoyote na kutokana na aibu iliyopo ndani ya hotuba ile wabunge Wa chadema wameanza kutofautiana na mwenyekiti wao anaowataka wasusie vikao vya bunge.

Nipo hapa Dodoma naisaka hotuba hiyo nikiipata nitaichapa upya ili kushare na nyie. Asubuhi wakati naingia mjini hapa nilikutana na gari ya Lisu maeneo ya bahi ikitokea mjini nafikiri huyu amekuwa mbunge Wa kwanza kusepa hapa. Juhudi za kufahamu mnajimu huyu anakoelekea zinaendelea kufanyika.


0 comments:

Post a Comment