Mtangazaji
wa ITV na redio, Salma Dakota hivi karibuni alipoteza fahamu baada ya
kufanyiwa ‘sapraizi’ ya kuvishwa pete ya uchumba na mpenzi wake, Gharibu
DumbaTukio hilo lilitokea kwenye Hoteli ya Protea iliyopo jijini Dar es
Salaam ambapo alikwenda bila kujua kuwa mtu wake huyo alikuwa na jambo
kubwa la kumfanyia. Ilielezwa kuwa, Salma akiwa hana hili wala lile,
alishangaa akivishwa pete ya dhahabu yenye kito cha Tanzanite ambayo
gharama yake ni takriban shilingi milioni 3.
Mtangazaji
wa ITV na redio, Salma Dakota akiwa kwenye pozi. Akizungumzia tukio
hilo mtangazaji huyo alisema: “Nilipata mshituko kwani sikutarajia na
ndiyo maana nikapatwa na hali ile. Namshukuru Mungu kwa hili
lililonitokea, ni jambo la heri na Mungu aniongoze katika safari hii ya
kuelekea kwenye maisha ya ndoa.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment