Friday, March 20, 2015

Shuga mummy atelekezwa na mvulana wake Uingereza

Mwanamke mmoja nchini Uingereza mwenye miaka 64 alitelekezwa na kuachwa na mvulana wake wa Kiafrika mwenye miaka 26 baada ya kumkamilishia taratibu za visa.

Mwanamke huyo mlemavu 64 ambaye alimpenda mvulana wa asili ya Tunisia 26 kupitia mitandao ya kijamii, alimkamilishia taratibu zote za kufika na kuishi Uingereza.
Patricia 64, alijuana na Mtunisia huyo katika tovuti ya mahusiano na kumpenda hatimaye kufanya taratibu za ndoa.
Patricia ambaye anaishi Midlands, alielezea namna alivyokua akitafuta mpenzi wa kuishi naye milele katika redio Channel 5 nchini Uingereza.
"Mwanzoni alionesha kuwa ana mapenzi ya dhati na kunishawishi kuwa miaka haimaanishi kitu zaidi ya tarakimu tu", alieleza Patricia.
Lakini Mondhler alipofika tu Uingereza alimtelekeza na kumuacha kizee huyo solemba.

0 comments:

Post a Comment