Weezy aliongeza kuwa wakati akitumikia kifungo hicho, Drake alimtembelea na kukiri kwa kusema, "Ndiyo, ni kweli. Usilale naye tena kama ulivyokuwa ukifanya awali maana tayari nimefanya naye mapenzi."
Wayne aliandika, "Huu ni upuuzi ambao mwanaume yeyote hasingependa kuusikia hasa akiwa gerezani. Labda, maana Mungu pekee ndiye ajuaye nini ningekifanya kama nisingekuwa gerezani kwa wakati huo."
Wayne ameelezea kwenye muswada huo kuwa, yeye na mpenzi wake walibishana sana, ndiyo maana Drake aliamua kumwambia ukweli kuwa "Usifanye nae mapenzi tena kama awali."
Lil alizidi kufunguka kuwa baada ya kuambiwa taarifa hiyo alijisikia vibaya mno na kuchukulia tukio hilo kuwa baya kuliko mengine yote aliyowahi kukutana nayo maishani.
Lil akizidi kumwaga ubuyu aliongeza kuwa "Kama mwanaume, ni wazi, kitu hicho kiliniuma sana na siyo kwa sababu alikuwa Drake, hata kama angekuwa mwanaume mwingine. Ingeniuma sawa."
0 comments:
Post a Comment