Ripoti kutoka nchini Marekani
zinasema uchunguzi uliofanywa na Wizara ya Sheria kuhusu tukio la mauaji
yaliyotekelezwa na Polisi dhidi ya Kijana mweusi mjini Ferguson
umebaini kuwepo kwa viashiria vya upendeleo na ubaguzi mjini humo kwenye
idara ya Polisi, mahakama na Mfumo wa Magereza.
Kijana mweusi , Michael Brown, alipigwa risasi na Askari wa kizungu.Maandamano yaliibuka mjini Missouri baada ya mauaji hayo, kisha baada ya jaji kuamua kutomshtaki Afisa wa Polisi
Matokeo ya Uchunguzi uliofanywa na Wizara ya Sheria yanatarajiwa kuchapishwa siku ya jumatano.

0 comments:
Post a Comment