Monday, March 2, 2015

indexMahmoud Ahmad Arusha
……………………………………………………………
Watanzania wametakiwa kujitolea kufanyakazi za jamii ikiwemo kujitokeza kwenye shughuli za Maendeleo kwa nguvu zao au kuchangia Maendeleo ya sehemu zao wanazoishi.
Kauli hiyo imetolewa na diwani wa Kata ya Unga Ltd Issa Said wakati aliposhirikiana na Wananchi wa kata hiyo kujaza kifusi na kutengeneza njia kuu ya wakazi wa mtaa wa Esso Mlimani ambayo ilikuwa ni kero kwa wakazi hao wakati wa kwenda na kurudi kwenye shighuli za ujenzi wa taifa.
Diwani Issa alisema kuwa  Maendeleo yeyote hayaji hivi hivi bila ya ushirikiano na Wananchi kwani  umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu hivyo watanzania wanatakiwa kujiletea Maendeleo kuanzia kwenye kaya zao hadi kwa umoja wao.
Alisema kuwa dhana ya Maendeleo ni pan asana na inatakiwa kuitenda kwa vitendo bila ya kunyoosheana vidole wa kubaguana kwa misingi ya vyama vya siasa kwani Maendeleo ni yetu sote bila kujali itikadi zetu.
Akawataka wakazi hao kushirikiana naye katika kuhakikisha kata yao inakuwa ya mfano wa kuigwa na kata zengine katika kujitoa na kujitolea kwa mambo ya Maendeleo.
Awali kabla ya kushiriki katika msaragambo huo diwani huyo alishirikiana na Wananchi katika kubeba kifusi eneo la Ostarbey cha kujazia shimo lililopo pembezoni mwa barabara ya waenda kwa miguu kwenye mtaa huo wa Esso Mlimani.
Mmoja wa wakazi wa kata hiyo Abdallah Soloka alisema kujitolea katika kazi za kujiletea Maendeleo ni wajibu wetu ila kumekuwa na kigugumizi kwa baadhi ya watendaji kutoshirikiana na Wananchi hususani kwenye shughuli za msaragambo kama ilivyokuwa awali wakati wa utawala wa awamu ya kwanza.
Soloka alisema kuwa ifike mahali watendaji wakawa wa kwanza kuwatembelea Wananchi ilikujua kero za maeneo yao badala ya kuwaachia madiwani kuzivumbua kwani wanakazi kubwa kwetu yakuhakikisha kero zetu zinafika kwa wakati kwenye mabaraza ya madiwani na kutatuliwa.

0 comments:

Post a Comment