Friday, March 20, 2015

 Akina mama wakiusimamisha msafara wa Komredi Kinana iliwaeleza tatizo la kutopatikana maji tangu wazaliwe katika Kijiji cha Shimbumbu, Jimbo la Arumeru Mashariki, mkoani Arusha.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akilakiwa na akina mama waliobeba ndoo tupu ikiwa ni ishara ya kuelezea tatizo la maji linalowakabili wakazi wa Kijiji cha Shimbumbu  Jimbo la Arumeru Mashariki,wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Wakazi wa eneo hilo wamedai kuwa wamekuwa na tatizo hilo la maji tangu wazaliwe kiasi cha kuwafanya walazimike kubadilishana maji na kokoto zinazotokana na kuuvunja mlima wa mawe uliopo kijijini hapo.

Komredi Kinana ambaye katika ziara yake ameambatana na Katibu wa Itikadiu na Uenezi, Nape Nnauye, amewaahidi wananchi wa eneo hilo kuwasaidia kukamilisha mradi wa maji utakaogharamiwa na Serikali ili mlima huo unusurike. Eneo hilo kwa hivi sasa linaoongozwa na Mbunge Joshua Nassari wa Chadema.
 Akina mama wakiwa na ndoo wakati wa mkutano na Komredi Kinana karibu na mlima unaopasuliwa mawe kupata kokoto za kubadilishana maji.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano uliofanyika Kata ya Mbungu, alikozaliwa yeye.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano uliofanyika Kata ya Mbuguni, alikozaliwa yeye.
 Wazee wa kabila la Wameru, wakimvisha mgolole ikiwa ni ishara ya kumkaribisha kuwa mzee wa kimila wa kabbila hilo.
 Nape akivishwa mgolole kiwa ni heshima ya wazee kumkaribisha kimila katika Kijiji cha Shimbungu
 Bibi kizee adelela Muungule (78)  akiwa miongoni mwa akina mama wa Kijiji cha Shimbungu, Jombo la Arumeru Mashariki. Bi Adelela amesema kuwa tangu utotoni wamekuwa wakiteseka kupata maji ambvapo walikuwa wanatembea umbali mrefu kuata maji katika mto mmoja uliopo mbali na kijiji hicho.

0 comments:

Post a Comment