MUIGIZAJI
wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ aliyekuwa na wafuasi wengi kwenye
Instagram, ameamua kujiondoa baada ya kushambuliwa kwa matusi na baadhi
ya watu kufuatia kifo cha mtu aliyewahi kuwa mpenzi wake.
Kufuatia
kifo cha kutatanisha cha Lusekelo Samson Mwandenga ‘Secky’, watu wengi
walianza kumtukana Lulu wakimhusisha pia na kifo hicho huku pia wakiweka
picha zinazomuonesha alipokuwa na marehemu.
Msanii mkongwe wa filamu, William Mtitu amefunguka na kuwataka watu kuacha kumshambulia Lulu kwa kitu ambacho hahusiki nacho.
Marehemu Lusekelo Samson Mwandenga 'Secky' enzi za uhai wake.
Msanii mkongwe wa filamu, William Mtitu amefunguka na kuwataka watu kuacha kumshambulia Lulu kwa kitu ambacho hahusiki nacho.
0 comments:
Post a Comment