Miaka
kadhaa nyuma aliibuka msanii mchanga na nyimbo kali na zilizogusa mioyo
ya wengi, hisia kali, mashairi yenye mpangilio na hata vina
vilivyosimama kwa unadhifu, walilia wenye kulia kwa tungo hizo,
wakafurahi wenye kufurahishwa na utunzi huo, vijana wakasema dah!,
mshikaji ni noumaa!, ndio, hayo ndo maneno yetu vijana tukimkubali mtu,
ila wazee nao wakasema Mungu amzidishie na kumbariki kijana huyu. Ndio,
maneno ya wakubwa dawa bwana, na Mungu kweli akatenda, kijana
akabarikiwa.
Kwa
mara ya kwanza nlimskia na wimbo wake ‘nenda kamwambie’, hatukukaa sawa
akaruka hewani tena na wimbo mzuri wa ‘Mbagala’, baada ya hapo
akafululiza na vibao kadhaa matata, ikiwemo ‘Nitarejea’, ‘Moyo wangu’ na
‘mawazo’, vyote vi kanigusa, si mimi peke yangu, ila wengi wetu
tuliguswa na tungo zake, ndio maana nikasema alipata baraka za vijana na
wazee.
Akalivuka
lile daraja reefu la hofu linaloogopwa na wengi, ‘kufeli’, na sasa
akawa ni mmoja wa waliomaarufu nchini, waliombeza wakamkubali,
waliompuuza wakamuona anafaa, hakuwa na baiskeli sasa akamiliki magari
ya kifahari, na mengine akayatoa zawadi kwa walioichezea bahati, bado
wazee wakambariki.
CHANZO : RAHA ZA WALIMWENGU
CHANZO : RAHA ZA WALIMWENGU

0 comments:
Post a Comment