Majibizano yakendelea.
Hamida Hassan
MSUTO! Mwanamke aliyetajwa kwa jina la Sina, mkazi wa Kawe jijini Dar amejikuta akisutwa mchana kweupe baada kumvujishia taarifa rafiki yake aitwaye Cheka Komba Mbegere kuwa wanawake wanaojiita Cash Money wanakwenda kumsuta, Risasi Mchanganyiko lilifuatilia hatua kwa hatua.
Mwanamke
aliyetajwa kwa jina la Sina (mwenye nguo nyekundu mbele kushoto), mkazi
wa Kawe jijini Dar akisutwa mchana kweupe na wanawake wanaojiita Cash
Money wanakwenda kumsuta. Tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo Cash
Money walichoshwa na tabia ya umbea wa Cheka ambaye ni memba wa kundi
hilo, ndipo walipoamua kumfungia kazi lakini akanusurika baada ya
kutonywa na Sina ndipo wamama hao waliobeba ngoma za vidumu vya maji
walipomsuta Sina kwa niaba ya Cheka.
Kwa mujibu wa Jamila ambaye naye ni memba wa Cash Money, Cheka alimgombanisha yeye na Sheila kwa kumwaambia kuwa wanatembea na bwana mmoja aitwaye Bubu pasipo kujijua.“Huyu mama amenifanyia kitu mbaya sana, alikuwa anakwenda kumwambia Sheila kuwa mimi natembea na mume wake ambapo tulikuwa tukigombana mara kwa mara na mwisho ndiyo hiyo juzi aliponivamia na kunipiga wakati nimelewa.
“Kwenye ule ugomvi Cheka naye alikuja kunichangia, kesho yake nilipozinduka nilikwenda kituo cha polisi Kawe na kushtaki, asivyo na haya akamuandikia SMS Sheila akimwambia waende kwa mganga ili eti waifute kesi,” alisema Jamila.
Baada ya kuona mambo yameshindakana kwa mganga, Sheila akaona bora amuombe msamaha Jamila ndipo walipomjua ‘mchawi’ wao ni Cheka kisha wakaungana kwenda kumsuta.
“Nilipoona mambo yamenifika shingoni nikaona nirudi kwa mwenzangu nimuombe msamaha tupatane, ndiyo nikamweleza mtu aliyekuwa akituchonganisha tukapanga siku ya kumsuta ambayo ndio leo lakini bahati yake akawa ametonywa akakimbia, tulichunguza tukabaini ametonywa na Sina ndipo naye tukamsuta barabara,” alisema Sheila.
Paparazi
wetu aliwashuhudia Cash Money wakimuimbia Sina nyimbo za kumsuta huku
wakipiga ngoma za vidumu vya maji kwa takriban nusu saa ambapo Sina
alileta vurugu kali ya kutaka kujinasua lakini hakufanikiwa.
“Hii ndiyo kiboko ya wambeya, kwa aliyeona fedheha hii kamwe hawezi kufanya umbeya wa aina yoyote,” alisikika shuhuda mmoja.
Baada ya kumalizika kwa tukio hilo, paparazi wetu alimvutia waya Cheka ili kumuuliza kama ni kweli alihusika kuwagombanisha Jamila na Sheila na sababu za yeye kutimka nyumbani hapo siku ya tukio.“Mimi nilikimbia kwa sababu walisema eti wamewaita waandishi waje wanisute lakini ukweli ni kwamba mimi sijawahi kuwachonganisha ila walipopigana nilikwenda kuwasuluhisha.
“Hata
hivyo wale hawanipendi kwa sababu nimejitoa kwenye kundi lao na
ninawadai hela zangu ndio maana wananichafua,” alisema Cheka. Hata
hivyo, Cash Money waliahidi kufanya msuto ‘party two’ muda wowote
watakapomtia mikononi Cheka wakidai wamechoshwa na tabia yake ya
kuwagombanisha watu.
Hamida Hassan
MSUTO! Mwanamke aliyetajwa kwa jina la Sina, mkazi wa Kawe jijini Dar amejikuta akisutwa mchana kweupe baada kumvujishia taarifa rafiki yake aitwaye Cheka Komba Mbegere kuwa wanawake wanaojiita Cash Money wanakwenda kumsuta, Risasi Mchanganyiko lilifuatilia hatua kwa hatua.
Kwa mujibu wa Jamila ambaye naye ni memba wa Cash Money, Cheka alimgombanisha yeye na Sheila kwa kumwaambia kuwa wanatembea na bwana mmoja aitwaye Bubu pasipo kujijua.“Huyu mama amenifanyia kitu mbaya sana, alikuwa anakwenda kumwambia Sheila kuwa mimi natembea na mume wake ambapo tulikuwa tukigombana mara kwa mara na mwisho ndiyo hiyo juzi aliponivamia na kunipiga wakati nimelewa.
“Kwenye ule ugomvi Cheka naye alikuja kunichangia, kesho yake nilipozinduka nilikwenda kituo cha polisi Kawe na kushtaki, asivyo na haya akamuandikia SMS Sheila akimwambia waende kwa mganga ili eti waifute kesi,” alisema Jamila.
Baada ya kuona mambo yameshindakana kwa mganga, Sheila akaona bora amuombe msamaha Jamila ndipo walipomjua ‘mchawi’ wao ni Cheka kisha wakaungana kwenda kumsuta.
“Nilipoona mambo yamenifika shingoni nikaona nirudi kwa mwenzangu nimuombe msamaha tupatane, ndiyo nikamweleza mtu aliyekuwa akituchonganisha tukapanga siku ya kumsuta ambayo ndio leo lakini bahati yake akawa ametonywa akakimbia, tulichunguza tukabaini ametonywa na Sina ndipo naye tukamsuta barabara,” alisema Sheila.
“Hii ndiyo kiboko ya wambeya, kwa aliyeona fedheha hii kamwe hawezi kufanya umbeya wa aina yoyote,” alisikika shuhuda mmoja.
Baada ya kumalizika kwa tukio hilo, paparazi wetu alimvutia waya Cheka ili kumuuliza kama ni kweli alihusika kuwagombanisha Jamila na Sheila na sababu za yeye kutimka nyumbani hapo siku ya tukio.“Mimi nilikimbia kwa sababu walisema eti wamewaita waandishi waje wanisute lakini ukweli ni kwamba mimi sijawahi kuwachonganisha ila walipopigana nilikwenda kuwasuluhisha.
0 comments:
Post a Comment