Rais wa zamani Mohammed Morsi
Makahama nchini Misri imemhukumu aliyekuwa rais wa zamani Mohammed
Morsi kifungo cha miaka 20 jela kutokana na kuuawa kwa waamdamanaji
wakati akiwa madarakani.
Hii nidyo hukumu ya kwanza kutolewa kwa Morsi tangu aondolewe madarakani, na moja ya hukumu zinazomuandama.
Morsi aliondolewa madarakani na jeshi mwaka 2013 kufuatia maandamano makubwa mitaani ya kupinga uongozi wake.
Yeye pamoja na viongozi wengine
wa Muslim Brotherhood walilaumiwa kwa kuwachochea wafuasi wao kumuua
mwandishi wa habari na waandamanaji wa upinzani wakati wa makabiliano
nje ya ikulu ya rais mwishoni mwa mwaka 2012.
Wakati umati ulipokusanyika nje ya ikulu bwana Morsi aliwaamrisha polisi kuwatawanya lakini wakakataa kufanya hivyo.
Baadaye
Muslim Brotherhood waliwaleta wafuasi wao ambapo watu 11 waliuawa
kwenye makabiliano, wengi kutoka kwa Muslim Brotherhood.
Kabla ya
kutolewa hukumu ya leo, Muslim Brotherhood walimlaumu rais wa sasa Abdul
Fatta al-Sisi kwa kutumia mahakama kama silaha.


0 comments:
Post a Comment