KING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ anatarajiwa kufanya maajabu Juni 6, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.
Akizungumzia na Mikito Nusunusu, mratibu wa burudani wa ukumbi huo, Abdallah Mrisho ‘Abby
Cool’ alisema kuwa siku hiyo Bella atauzindua wimbo wake mpya wa Nashindwa akishirikiana na bendi yake ya Malaika Music.
“Siku hiyo atapiga live, mara ya mwisho Bella kupiga shoo ya kihistoria Dar Live ilikuwa Sikukuu ya Wapendanao ambapo aliwaonjesha kidogo wimbo huo, lakinin sasa ataupiga mwanzo mwisho,” alisema Abby Cool.
0 comments:
Post a Comment