Kumekuwa
na madai kuwa, mwanadada Husna Sajent ameolewa na msanii mwenzake wa
filamu, Salim Ahmed ‘Gabo’ lakini wenyewe wamekuwa wakikanusha! Hata
hivyo, juzikati Maimartha Jesse ‘Mai’ alimwaga mchele mbele ya kuku kwa
kumuita Husna ‘Mrs Gabo’.
Mai
alifanya hivyo pale alipokuwa akiwatambulisha mastaa waliohudhuria
sherehe ya ‘baby shower’ ya Aunt Ezekiel iliyofanyika Mwendopolepole,
Bagamoyo mkoani Pwani.
Katika utambulisho huo, Mai alimuita Husna ‘Mrs Gabo’ akimaanisha na si kwa utani, hali iliyowafanya watu kuanza kunong’ona kwa chini na kumuacha Husna akicheka asijue namna ya kuua soo.
Msanii wa filamu za Kibongo, Husna Sajent.
“Si mwenyewe anasema ile picha iliyovuja akionekana kafunga ndoa na Gabo ni filamu, sasa kumbe watu wake wa karibu wanajua ukweli, mh! Makubwa,” alisikika akisema dada mmoja aliyekuwa eneo hilo la sherehe.
Katika utambulisho huo, Mai alimuita Husna ‘Mrs Gabo’ akimaanisha na si kwa utani, hali iliyowafanya watu kuanza kunong’ona kwa chini na kumuacha Husna akicheka asijue namna ya kuua soo.
“Si mwenyewe anasema ile picha iliyovuja akionekana kafunga ndoa na Gabo ni filamu, sasa kumbe watu wake wa karibu wanajua ukweli, mh! Makubwa,” alisikika akisema dada mmoja aliyekuwa eneo hilo la sherehe.
0 comments:
Post a Comment