Msanii wa kizazi kipya toka kundi la Weusi Lord Eyes na mwanzilishi wa kundi la Nako2Nako ameshuka kimuziki kutokana na jamii kukasirishwa na matendo yake ya utovu wa nidhamu.Juzi juzi alitoa wimbo wa kwanini aliomshirikisha GNako na mwanadada Mwasiti akijaribu kueleza jamii kwanini yanatokea lakini haujafanya vizuri.Ray C alimtaja live kwenye kipindi cha Mkasi kua alifundishwa madawa na msanii huyu.
Msanii huyo mwaka jana alikumbwa na mikasa ya wizi wa vifaa vya magari power window jijini Dar es Saalam na Arusha moja ikiwa gari ya msanii mwenzake Ommy Dimpoz baada ya kesi kuisha akatoa nyimbo ya mapito na Damian Soul.Kundi hilo la Nako2Nako linawasanii wawili wenye kusadikika kutumia madawa ya kulevya Lord Eyes na Ibra da Hustler ambaye amepotea kabisa kwenye gemu.


0 comments:
Post a Comment