Meya wa mji wa Boston Martin Walsh
amesema kuwa ana matumaini kuwa hukumu ya kifo aliyopewa mshambuliaji
kwenye mbio za Boston Marathon itawapa nafuu wale wote walioathiriwa na
shambulizi hilo.
Iliwachukua majaji saa 14 kuamua ikiwa Dzhokhar Tsarnaev atauawa kwa kudungwa sindano ya sumu badala ya kupewa kifungo cha maisha.
Waathiriwa kadha walielezea kuridhika kwao wakisema kuwa uamuzi huo utawawezesha kuendela na maisha yao.
Wengi wanahofu kuwa ikiwa rufaa itakatwa, itawaongezea machungu zaidi moyoni.

0 comments:
Post a Comment