Habari
kutoka nyumba ya jirani nchini Uganda ikufikie kwamba aliyekuwa mume wa
mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan
‘Zari The Boss Lady’, tajiri Ivan Ssemwanga anadaiwa kunasa penzi la
shosti wa kufa na kuzikana wa mkewe huyo aitwaye Stella Nankya, Ijumaa
Wikienda limetonywa.
Aliyekuwa
mume wa Zari akiwa na mpenzi wake mpya ambaye ni shosti wa kufa na
kuzikana wa Zari. Ubuyu kutoka jijini Kampala nchini humo ulidadavua
kwamba, Ivan na Stella ambaye ni modo maarufu wa Uganda na Afrika Kusini
‘Sauzi’, hivi karibuni wamekuwa wakijiachia kimalovee kwa raha zao.
Zari
akiwa na shosti wake Stella Nankya ambaye ni modo maarufu wa Uganda na
Afrika Kusini ‘Sauzi’. Tukio la juzikati lililoacha gumzo ni pale wawili
hao waliponaswa wakiwa wamegandana kimahaba kwenye Ukumbi wa Ekitone
uliopo Pretoria nchini Afrika Kusini ambapo kulikuwa na tamasha la
muziki.
Modo
maarufu wa Uganda na Afrika Kusini ‘Sauzi’ Stella Nankya akiwa katika
pozi. “Walikaa pamoja, walijiachia pamoja ziro ‘distansi’ kwani hakukuwa
na kitu cha kuwatenganisha kati yao. Kwa kweli walionekana ‘kapo’ ya
kupendeza mno,” alisema shuhuda wa tukio hilo na kukaririwa na gazeti
moja la nchini Uganda.
Kufuatia urafiki wa Stella na Zari walivyokuwa wameshibana, mashabiki wao wamekuwa na maoni tofauti huku Stella akionekana msaliti kwa Zari.
Habari nyingine zilidai kwamba, Ivan ameamua kufanya hivyo ikiwa kama kisasi au kumrusha roho Zari aliyezaa naye watoto watatu ambapo anatarajia kumzalia Diamond siku chache zijazo.
Ilielezwa kuwa, Stella alipoulizwa kwa nini ameamua kumsaliti rafiki yake Zari kwa kutembea na Ivan alisema kwa kifupi:
“Sitaki kuwa karibu na mtu mkavu (Zari), na mimi nimeamua kuwa mkavu.”
Zari au mama kijacho na Stella walikuwa ni marafiki wakubwa ambapo kuna wakati Zari alimpa sapoti ya nguvu Stella alipokwenda kuiwakilisha Uganda kwenye mashindano ya urembo ya Miss Asia Pacific huko Seoul nchini Korea Kusini ambapo walisafiri wote.

0 comments:
Post a Comment