Imelda Mtema
HAPATOSHI!
Mkongwe wa sinema za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na mwigizaji
mwenzake, Halima Yahaya ‘Davina’ nusura wazichape kavukavu katika Ukumbi
wa Mlimani City, jijini Dar baada ya Ray kudaiwa kumshika mwenzake huyo
sehemu nyeti, Risasi Mchanganyiko lina mchapo kamili.
Staa
wa Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’. Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho
kilikuwa shuhuda wa tukio hilo, Davina alikuwa amekaa na wasanii wengine
pamoja na Mlezi wa Bongo Movies, mama Loraa wakipata vinywaji ndipo Ray
alipofika na kuharibu shughuli.
“Wakati Davina anaendelea kupata kinywaji na mama Loraa, alitokea Ray akiwa tayari ‘ameshakula vyombo’ na kumshika Davina kalio kitendo kilishomkasirisha sana msanii huyo na kuanza kumcharukia Ray,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
Halima
Yahaya ‘Davina. “Davina alinyanyua glasi ya kinywaji chake, akammwagia
Ray huku akimuuliza kwa nini alimshika makalio ndipo Ray naye
alipopandisha hadi wakataka kukunjana.”
Baada ya vurugu hizo kuanza kushika kasi, alitokea mwigizaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na wenzake ambao waliwasihi wawili hao waachane na mambo hayo.
Baada ya kupata habari hiyo, gazeti hili liliwatafuta wahusika ambapo lilianza na Davina.
“Jamani mi nafikiri nisizungumzie hilo tukio maana naona ni la aibu, si kitendo kizuri na kinaniumiza mno kwa maana ni udhalilishaji mno na kwa nini mtu akufanyie hivyo?,” alisema Davina. Simu ya Ray iliita bila kupokelewa.
“Wakati Davina anaendelea kupata kinywaji na mama Loraa, alitokea Ray akiwa tayari ‘ameshakula vyombo’ na kumshika Davina kalio kitendo kilishomkasirisha sana msanii huyo na kuanza kumcharukia Ray,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
Baada ya vurugu hizo kuanza kushika kasi, alitokea mwigizaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na wenzake ambao waliwasihi wawili hao waachane na mambo hayo.
Baada ya kupata habari hiyo, gazeti hili liliwatafuta wahusika ambapo lilianza na Davina.
“Jamani mi nafikiri nisizungumzie hilo tukio maana naona ni la aibu, si kitendo kizuri na kinaniumiza mno kwa maana ni udhalilishaji mno na kwa nini mtu akufanyie hivyo?,” alisema Davina. Simu ya Ray iliita bila kupokelewa.
0 comments:
Post a Comment