STAA
wa filamu Bongo, Irene Paul ‘Smart Girl’ amezua mshangao baada ya
kupiga mayowe huku akirusha mikono kushangilia tuzo aliyopata jambo
lililozua miguno kwa waliomshuhudia.
Msanii huyo alipata tuzo hiyo kwa kipengele cha The
Best Actress (Supporting Role) kupitia Filamu ya Never Give Up
aliyoshirikiana na msanii kutoka Nigeria, Joseph Van Vicker na
kuonekana kuchanganyikiwa namna hiyo. Baada ya kuchukua tuzo hiyo, ‘kiruka njia’ wetu alimfuata na kumuuliza kulikoni aonekane kupagawa kwa kiwango hicho ambapo alisema kutokana na ugumu wa kipengele hicho kwani alikuwa akichuana na watu anaowaheshimu sana katika tasnia ya filamu, alioamini wana kiwango cha juu kuliko yeye hivyo hakuamini kilichokuwa kinatokea kwa wakati huo.
0 comments:
Post a Comment