
Hakuna ubishi kua kwa sasa diamond platnumz ndie msanii anae ongoza kupigwa vita kuliko msanii yeyote hapa nchini.
Vita
hiyo ina ongozwa na baadhi ya walio wahi kuwa wapenzi wake pia na
mahasimu wake wa kimuziki (wasanii wengine) kupitia mashabiki zao.
Sawa
ni jambo la kawaida kwa wasanii wakubwa duniani na mastar wengine kama
wachezaji,maboxer pamoja na waigizaji kuwa na maadui hili
linathibitishwa na mfano wasanii kadhaa wa kimarekani walivyo na maadui
mpaka inafikia kupigana risasi mfano 2pac,BIG,50cent,mayweather na
wengine kibao.
Sababu kubwa za
diamond kuanzishiwa vita "maalum" ili ashuke kimuziki na kimafanikio ni
kutokana na maneno ya wengi eti kua anaringa,anadharau,ana nyodo,ana
mamneno ya shombo,ana ropoka sana,mtoto wa uswahili,hajasoma,mchawi na
visababu kedekede.
Wadadisi wa mambo
wanasema kua chuki dhidi ya diamond si tu inatokana na sababu zilizo
tajwa hapo juu bali inaenda mbali zaidi mapaka kwa team nzima ya diamond
hasa mameneja wake.
0 comments:
Post a Comment