Wednesday, June 10, 2015

BARUA YA WAZI KWA KAKA DISMAS LYASSA.

Kuna watu ambao nilikua nikiwaamini na kujifunza mengi kutoka kwao, lakini once upon a time they proved me wrong. Mmoja wapo ni kaka Dismas Lyassa. Huyu nilimfahamu tangu akiwa GPL wakati ule akiandika kuhusu Saikolojia na Utafiti.


Ilikua mwanzoni mwa miaka ya 2000. Nilikua nikitoroka shule natembea zaidi ya kilomita 20 kwa mguu kwenda mjini kununua gazeti ili nisome story za Shigongo na makala za Dismass Lyassa.
Na kwa hakika siwezi kuyapuuzia maandiko yao. Ni wazi yapo mengi niliyojifunza kutokana na makala za Lyassa na bado naamini ni mwandishi mzuri hata sasa.

Tatizo la Lyassa ni alipojiingiza kwenye siasa. Akachagua CCM. Najua kila mtu ana haki ya kuchagua chama akipendacho.. na ninaheshimu maamuzi ya mtu yeyote kujiunga na chama chochote cha siasa, thats why nina marafiki wengi walioko CCM, CUF, NCCR na vyama vingine.
The "issue" ni kuwa Lyassa ameingia kwenye siasa kwa kujipendekeza. Na hiki ndicho kimenifanya nikapoteza imani nae. Anajaribu kwa kila hali kuponda upinzani (hasa CHADEMA) na kuonesha chama chake CCM ni bora hata pale ambapo wananchi wanakiona si bora.
Kibaya zaidi ni kuwa anafanya hivyo kwa maslahi. Yani anaponda CHADEMA na kusifia CCM si kwa sababu anaamini CCM inaweza kuleta mabadiliko, bali kwa sababu anaamini kwa kufanya hivyo atapata cheo fulani ndani ya chama chake au serikali.
Nimekuwa nikifuatilia maandiko yake ya karibuni hasa kuhusiana na jimbo la Kilombero ambapo anatarajia kugombea ubunge ikiwa chama chake kitampitisha. Nilichogundua ni kuwa kaka Dismass anawinda mno madaraka kuliko anavyowinda kuwatumikia watu.
Yani anatamani kuwa kiongozi zaidi.. kuwa mheshimiwa fulani.. kuliko anavyotamani kuwatumikia watu.
Nimelazimika kuandika hivyo kutokana na barua aliyoiandika Dismass mwaka 2013 akiomba cheo cha Ukuu wa wilaya kwa Mwigulu Nchemba. Barua hiyo iliyonaswa na gazeti la MAWIO inaonesha Dismas akimuomba Mwigulu ampigie kifua kwa 'JK' apate ukuu wa wilaya.
Ktk kuhakikisha azma yake inafanikiwa Dismas anamsifia Mwigulu kwa sifa kedekede ikiwa ni pamoja na kumhakikishia kuwa bado anakubalika Iramba. Hakuishia hapo tu Dismas anamponda DC aliyekuwepo Kilombero kwa kuondolewa na kurudishwa jeshini.
Habari hiyo ilichapishwa katika MAWIO ya tar.15 August 2013 na Dismas hajawahi kukanusha taarifa hiyo.
Sasa mimi leo naomba nimuulize kaka yangu Dismas je habari ile ilikua ya kweli au lah. Kama ni kweli kwanini alifanya hivyo, na kama si kweli je amechukua hatua gani kwa gazeti la MAWIO?
Kwa wale ambao walishindwa kuisoma habari hiyo kwny gazeti la MAWIO la 15/08/2013 wanaweza kusoma hapa chini nimeattach.
"AOMBA UKUU WA WILAYA KWA MWIGULU..
Mmoja wa wahariri wa gazeti la mwananchi, Dismas Lyasa,ameomba kazi ya ukuu wa wilaya kwa Mwigulu Nchemba,taarifa ndani ya CCM na serikali zinasema, Mwigulu amevujisha taarifa za Lyasa kutaka kupewa nafasi hiyo kwa marafiki zake.
Pamoja na kuwa Mwigulu hana uwezo wa kutoa kaz ya nafas hiyo, isipokuwa ana ushawishi kwa rais na pinda ambae ndio wenye uwezo wa kutoa kazi nafasi hiyo.
Akiandika kwa Mwigulu, agosti 3 jumamosi mwaka huu,Lyassa ambae ni mhariri wa kijarida cha ''habari ndani ya habari'' katika gazeti lka Mwananchi ameomba,''.... ningefurahi kupata fursa ya kuwa DC wa kilombero''
Katika maombi yake Lyasa ameambatanisha cv na amemhakikishia Mwigulu kuwa yuko tayari kufanya kazi nae bega kwa bega na kwa staili yoyote .....
 
Lyasa anaandika,''nasikia kuna DC amerudishwa jeshini, na kwamba angefurahi kupata fursa ya kuwa mkuu wa wilaya huko...
AKiandika kwa njia ya kubembeleza,lyasa amesema, '' ninazo sifa za kuwa mkuu wa wilaya ya kilombero.. Lyasa anasema,naamin kama dc wa sasa ameshindwa kusaidia chochote,na ndio maana kiti cha udiwani Ifakara mjini kimeenda CHADEMA..anasema anayo mikakati mizito ya kuhakikisha kuwa CCM inakubalika kilombero,hivyo anaomba Mwigulu amsaidie kufanikisha mikakati yake hiyo.

Lyasa pia anamtaadharisha Mwigulu kuwa, Dk Kitila Mkumbo,mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA ametangaza kugombea ubunge jimboni kwake (kwa mwigulu), mwaka 2015,lakin Lyasa akimpa moyo kuwa bado ana nguvu...

Source: MAWIO 15/08/2013."
MY TAKE.!
Dismas aachane tu na siasa afanye mambo mengine. Najua the man is capable and competent but not in politics. Siasa awaachie wanaoiweza.!

  • Erick M. Walter Kweli wewe ni critical thinker!! mimi nilishawahi kuumuliza maswali magumu katika post zake mbalimbali hapa fb lkn hakuwa na majibu ya kutosha!! waandishi wengi badala ya kutumia kalamu zao kuwaelimisha wananchi sifa za viongozi bora wao wanasifia viongozi dhaifu ili wapate vyeo!! kama ilivyo policcm,pia kuna wanahabariccm!!
    Like · Reply · 3 · 3 hrs
  • Rawasen Munisi Exclusive Letter
    Haika Malisa
  • Manawa Bukwimba Shytown Tatizo LA lyasa ni njaa
  • Gasper Mrosso Na mm niliinasa barua yake......Lyassa anajichafua mwenyewe
    Like · Reply · 1 · 2 hrs
  • Steven I. Mshiu Hahahahah...njaa. mkiwapa ikulu watu wenye uchu wa madaraka, si ajabu tunaamka siku moja tunakuta ameshaiuza.
    Like · Reply · 1 hr
  • Jordan Benjamin Wasonga Huyu hana tofauti na Cyprian Musiba Wa Chanel Ten, ambaye naye anatafuta ukuu wa wilaya akidhani makongoro atakuwa Rais.... Hvi ukuu wa wilaya unaombwa kweli?
    Like · Reply · 1 · 1 hr
  • Lyhni M. Senior #Comrade Malisa Godlisten, umetenga haki. Na kama kuna utukufu uliokuwa unamiminika basi ni wakati unaandika makala hii. Uandishi wa #ukasuku na #uimbaji wa yale ya watawala na dhambi ya waandishi. Ni kinyume na halali ya macho na masikio. Ieleweke kuw...See More
    Like · Reply · 1 hr
  • Buberwa Mwemezi Huyu jamaa aliwahi kugombea pia Urais wa shrikisho la vyama vya wafanyakazi (TUCTA) ila aliambulia patupu,anatafuta ulaji kwa nguvu baada ya kushindwa akaja na pendekezo kwa viongozi la kuanzishwa kitengo chake cha habar ndan ya shirikisho hilo.Nadhan aache haya mambo ataaibika zaidi.
    Like · Reply · 1 hr
  • Salum Abdi Anajisifu kuwa anapigiwa kampeni na wananchi bila ya yy kufika huko pia kaanza kuchangisha wananchi.
    Like · Reply · 1 hr
  • Asumwisye Edward Mbwile Jamaa yupo after money sana...kuna kipindi nilimuomba anisaidie kutafuta schoralship nje ya nchi akakubali lakini pesa aliyotaka nimlipe daaah nikakata tamaa
    Like · Reply · 1 hr
  • Baraka Masindoki Huyu jamaa alinifanya niache kununua gazeti la mwananchi kwa miezi 2, baada ya kusoma makala ya mawio..uzuri Malisa Godlisten
  • Diana Nicetas Jamani Watanzania wenzangu watu kama hawa wenye kutaka maslahi yake kwanza yani oesa mbele sio wa kuwapa hata Mwenyekiti wa serikali za mitaa. Na wapi wengi maana tunaishi nao kwenye kazi tumefanya nao. Ebu jaribuni kuangalia historia zao za nyuma. Ili tupate viongozi bora wenye hofu ya MUNGU.

0 comments:

Post a Comment