Posted by Williammalecela.com on Wednesday, June 10, 2015
Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madame'.NI shiida! Siku chache baada ya msanii wa muziki wa
kizazi kipya nchini, Esterlina Sanga ‘Linah’ kulalamika juu ya kitendo
cha Wema Sepetu ‘Madame’ kumchukua aliyekuwa bwana’ake Nangari Kombo,
muigizaji huyo ameibuka na kutoa maneno yanayoashiria kejeli, kuwa aache
presha, kwani zile ni picha tu!Katika
gazeti la Risasi Jumamosi, toleo lililopita, iliripotiwa na kuchapishwa
habari na picha zilizomuonyesha Madame akiwa amepozi kitandani na kijana
huyo, aliyepata umaarufu baada ya kuingia ndani ya eneo la kuchezea
katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam mwaka 2010, wakati wa mechi
kati ya Brazil na Taifa Stars na kumkumbatia kiungo nyota wa mabingwa
hao wa zamani wa dunia, Kaka.
0 comments:
Post a Comment