Mwanamke mmoja nchini Nigeria ametangaza kupitia
redio kuwa anatafuta mume, akisema atampa gari na
nyumba. Mamia ya wanaume walifurika kituo cha radio
cha Freedom, mjini Kano ambapo polisi walilazimika
kuitwa kutuliza watu. Msichana huyo, Zainab
Abdulmalik, 22, amesema alikuwa amekasirishwa mno
na 'boyfriend' wake wa zamani. Mtangazaji wa redio - Nasiru Zango- ameiambia BBC kuwa Zainab alichagua mchumba kutoka katika mlolongo mrefu wa wanaume waliokuwa wamejipanga nje ya kituo cha redio na kuondoka.

0 comments:
Post a Comment