Friday, June 19, 2015


"Unapofunga sukari na maji hupungua mwilini mwako.
Ndio ikasuniwa kuftari tende kwani ina uwezo wa kurejesha sukari ilopotea siku nzima. Kisha fatiliza chakula chepesi na laini kwanza kama chapati za maji, ndizi na vinginevyo kwani utumbo unakuwa umesinyaa si vyema kuupa vyakula vigumu.


 

Usile mpaka ushibe sana utajikuta unachoka sana hata ibada itakushinda. Kula kidogo pumzika kisha utaendelea taratibu.
Tafadhali usichanganye maji baridi na chai au uji ukanywa kwa pamoja inahatarisha afya yako.
 

Epuka Soda au juice za viwandani kwani inawekwa madawa mengi na baadhi sio matunda halisi pia sukari inayotumika ina madhara na badala kunywa juice halisi ilotengenezwa kawaida (fresh juice).
Kumbuka tunafunga tupate afya na sio tuongeze maradhi"

0 comments:

Post a Comment