Pombe
zitamtoa roho! Unywaji wa pombe kupita kiasi anaoufanya staa wa sinema
za Kibongo, Blandina William Chagula ‘Johari’ umetafsiriwa kama
kujihatarisha kiafya baada ya hivi karibuni kunaswa mchana wa jua la
utosini akifakamia ulabu huku akionekana kuzidiwa, jambo lililozua
minong’ono kwa baadhi ya watu, Risasi Mchanganyiko lilimnyatia.
Akiwa
‘ametumbua’ macho, mwandishi wetu alimfuatilia mhudumu huyo na kubaini
kinywaji kilichoagizwa na Johari ni pombe ndipo akaweka sawa kamera yake
kwa ajili ya lolote. Kwa kasi, paparazi wetu alimfotoa picha za mbali
na kwa tahadhari ya kutoshtukiwa kabla ya kuondoka eneo la tukio.Mwandishi wetu hakuweza kumfuata Johari mahali alipoketi na badala yake aliondoka kisha kumpigia simu ambapo awali alikataa kutokuwepo kwenye baa hiyo lakini baada ya kubanwa kwa hoja nzito, alijikuta akikiri na kufunguka jambo jipya.
“Dah! Ulikuwa umekaa wapi? Lakini siyo mawazo nimeamua tu kupumzika na kazi kwa leo hivyo nikaona si vibaya kama nitajiburudisha kwa kinywaji hiki,” alisema Johari.
0 comments:
Post a Comment