Wednesday, June 17, 2015

Kumetokea ajali ya aina yake jioni hii mjini Shinyanga ambapo gari ndogo aina ya RAV4 yenye namba za usajili T167 ATW imegonga nyumba katika mtaa wa Mnara wa Voda mjini Shinyanga.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 11 jioni ambapo mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde1 blog kuwa gari hiyo ilikuwa inaendeshwa na watu wawili wanaodaiwa kuwa walikuwa wanajifunza kuendesha tena kwa mwendo kasi ndipo gari ikawashinda na kupoteza mwelekeo kisha kugonga nyumba hiyo na kusababisha uharibifu mkubwa.
Gari hiyo imeharibu vibaya Chumba cha mpangaji aliyejulikana kwa jina la Fatuma kuharibu vifaa mbalimbali zikiwemo TV katika chumba hicho na chumba cha jirani cha Fundi Sonara aliyejulikana kwa jina la Ally Salum.
Hata hivyo hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa na wahusika wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi na mmliki wa gari hiyo bado hajajulikana.
Mwandishi wetu Kadama Malunde,alifika eneo la tukio,ametuletea picha zifuatazo

Gari ikiwa imegonga nyumba hiyo

Gari ikiwa chumbani
Muonekano wa gari hiyo kwa ukaribu 




Askari wa usalama barabarani wakiwa eneo la tukio wakiwajibika
Gari ikiwa ndani ya chumba 




Mashuhuda wa tukio hilo wakiwaeleza askari polisi wa usalama barabarani namna ajali hiyo ilivyotokea
Katikati ya hiyo miti ndipo ilipopita gari hiyo ikiwa katika mwendo kasi kisha kugonga nyumba hiyo 

ndani ya chumba cha mpangaji Fatuma


Chumba cha mpangaji Fatuma kikiwa kimeharibika vibaya
Fundi Sonara Ally Salum akionesha ilipokuwa TV yake iliyoharibika



Fundi Sonara Ally Salum akionesha akitafakari jambo nje ya chumba chake



Askari wakitafakari namna ya kuiondoa gari hiyo eneo la tukio

Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio baada ya gari hiyo kuondolewa kwenye chumba

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

0 comments:

Post a Comment