DAKTARI wa Kitengo cha Sayansi na Tiba Asili kilichopo Mbezi-Afrikana, Dokta Fadhili Emily, amemnunulia baiskeli ya kubebea mtoto, mpenzi wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kama zawadi pindi atakapojifungua.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko akiwa nchini Sweden alikoenda kwa ziara binafsi, Dokta Fadhili alisema kwa kutambua yeye ni mtu wa Kigoma anakotokea Diamond, ameona amnunulie shemeji yake huyo baiskeli hiyo ambayo kwa mujibu wake, ina thamani ya shilingi milioni 5 za Kitanzania.
Zari anatarajiwa kujifungua kati ya Agosti au Septemba, mwaka huu ambapo ujio wa mtoto huyo umekuwa ukitengeneza vichwa vya habari kila kukicha.
0 comments:
Post a Comment